Dubrisi (pia: Dubricius, Dubric, Dybrig, Dyfrig, Devereux; Madley, Uingereza, 465 hivi - Kisiwa cha Bardsey, Welisi, 550 hivi) alikuwa mmonaki msomi anayetajwa kama mwanzilishi na abati wa monasteri za huko Hentland na Moccas halafu kama askofu wa Llandaff [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Novemba[2].